KONGAMANO LA 13 LA MAOMBI YA KITAIFA - DODOMA (UDOM) - 2021
NA MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE
TAREHE 18 AUGUST, 2021DAY-2,SESSION-2
KUOMBA KWA AJILI YA UCHUMI
AGENDA:-YESU AWE MDHAMINI WAKO KIUCHUMI KITAIFA.
Waebrania 7: 22
basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.
Mungu anaposhughulika kuwasaidia watu kiuchumi huwa anawasaidia kiagano ili wasaidike kwa namna ya kudumu. Maana ikiwa nje ya agano haiwi ya kudumu.
Nuhu alipotoka kwenye Safina ili Mungu amsaidie yeye ilibidi amsaidie kiagano. Mwanzo 8. Hii liligusa kiupana sana ili aweze kusaidiwa.
Abrahamu alisaidiwa kiuchumi na Mungu kiagano. Mungu alimwambia katika kukubariki nitakubariki.
Pia angalia habari za Isaka katika Mwanzo 26. Njaa ilitokea tena kama kipindi cha Ibrahimu. Isaka alienda kwa Abimaleki ili aende Misri. Mungu alimtokea Isaka akamwambia yeye ni Mungu wa agano wa baba yake.
Ibrahimu alipoingia katika agano aliwaingiza na watoto wake. Isaka alikuwa hamfahamu Mungu wa baba yake kiagano. Lakini mpaka alipoingia katika agano na Mungu wa baba yake. Baada ya kuchimba kisima cha tatu ndipo Isaka akajenga madhabahu.
Yakobo alipopata shida ya njaa na Yusufu ndiye aliyekuwa kabeba majibu ya uchumi wao. Kwa hiyo ilibidi wamfuate mahali alipo. Na yeye Yusufu aliwasaidia kiagano.
Wana Israeli nao walipopata shida ya mazingira ya kazi yaani utumwa. Walimlilia Mungu maana walikuwa wanaomba ili wabadilishiwe mazingira ya kazi. Kwa hiyo Mungu alitazama agano haisemi alijibu maombi yao. Aliwasaidia kiagano kabisa. Kutoka 2:24
Ukiomba kwa Mungu ili awe mdhamini wako kiuchumi kiagano uwe na uhakika atabadilisha maisha yako kabisa.
Mungu alianza kujibu tatizo la wana Israeli walipokuwa Misri aliwajibu kiagano kabisa. Mungu alipanga watoke baada ya miaka 400. Lakini wao walitoka baada ya miaka 430. Yaani miaka 30 ya kubishana Misri ambapo walitoka miaka 430. Pia walipewa adhabu miaka 40 jangwani. Kwa hiyo mpaka wanaingia Kaaniani ilikuwa ni miaka 470 imepita. (430+40=470)
Mahali popote ambapo wana Israel waliharibu mahusiano yao na Mungu walikwama. Mpaka leo hata katika agano jipya ni vivyo hivyo. Kabidhi kila kitu chako kwa Mungu.
Kwa wengine waliofanya hivyo watu wamempa Mungu kila kitu. Na kuna wengine ambao bado au wamempa Mungu tu sehemu.
Yesu alikuwa masikini ili sisi tuwe matajiri katika yeye. Na baraka za Mungu zipo kiagano na huwa zinagusa eneo pana. Mungu anamtajirisha mtu kwa ajili ya kuimarisha agano.
Makanisa mengi yanapata shida kiuchumi kwa sababu hawajafunga agano na Mungu.
Je unaelewa kwanini Mungu alimwambia Ibrahimu amtoe Isaka ili awe sadaka?. Kwa hiyo ilibidi amtoe ili awe wa Mungu. Mungu alisema sasa najua kuwa unanipenda maana hukunizuilia mwanao wa pekee.
Hapo alikuwa unamuelewa aliposema sasa nilikuwa nasubiri ili awe wake. Mungu alisema sasa katika kuiubariki nitakubariki. Mungu akikupa kazi anataka kazi umpe tena. Anataka ukambidhi tena.
Isaka aliyetwa mlima Moria kwa ajili ya sadaka alikuwa wa Ibrahimu. Isaka aliyetoka mlima Moria na kurudi na Ibrahimu alikiwa ni wa Mungu ila sasa yupo mikononi mwa Ibrahimu.
Sasa chukulia Isaka ni mradi, maana yake kama Isaka ana deni, linakuwa ni la Mungu naye. Maama hata katika sheria za duniani hapa mtu akinunua kampuni ananunua na mali na madeni yote ya hiyo kampuni.
USHUHUDA
Kitabu cha kwanza kutoa ni Kusamehe na kusahau. Baada ya kukiandikia kabla ya kukitoa tulitakiwa kutoa fedha Downpayment ya Tsh 17,500. Mshahara wangu wa wakati huo ilikuwa ni Tsh 1,000. Ilikuwa ni jaribu kubwa sana maana kiasi hicho kilikuwa ni kikubwa sana kuweza kutoa ukilinganisha na kipato changu cha wakati huo.
Kwa hiyo tulimuomba Mungu akatufungulia mlango na tulipata fedha hiyo. Sasa baada ya kulipa wale wachapishaji wakaanza kuchelewesha bila sababu kumaliza kazi.
Nikawa naomba ili Mungu aingilie kati, Yesu alisema nipe nikabidhi hili suala kama wikili.
Basi nikawaandikia barua kuwa ndani ya siku 2 inatakiwa wawe wametoa kitabu bila hivyo wakati wangu atalipeleka hilo suala katika vyombo vya sheria.
Niliwapeleka barua kwa dispatch book ili wasaini kabisa ikuwa wamepokea. Nikaandika na kule chini Nakala kwa Wakili JC. (Yaani Jesus Christ).
Baada ya kuandika hiyo barua nikaibandika mikono na kumkabidhi Yesu ili aishugulikie.
Siku hiyo hiyo akaja Maneja wa masomo nyumbani kwangu wa kiwanda hicho.Akasema sasa Mwakasege suala hili tupelekane katika vyombo vya sheria? Nikawaambia ili mpone leteni vitabu ndani ya siku 2 bila hivyo wakili wangu ataaanza kulishughulikia jambo hili.
Basi ndani ya siku 2 wakaleta nakala za vitabu vyote kama tulivyokubaliana. Maana sikutaka kuwaambia Wakili JC ni nani ili wasije mpata. Maana nina uhakika walitafuta mjini na walimkosa.
MAMBO MANNE YA KUOMBEA.
Kabidhi kwa biashara/kazi yako kwa Mungu
Tuombee soko sawa sawa Ufunuo 5:9-10
Kazi za kufanya. Mungu akupe mawazo ya kitu cha kufanya ili kukuongezea kipato.
Ombea akina Zakayo ili wasije wakatoza zaidi. Maana kama wako akina Zakayo katika mfumo wa kodi na wanatoza zaidi ili Mungu atusaidie wafanye kazi vizuri bila kutoza zaidi na kuomba rushwa.
Chukua agenda hizi nenda nazo kwa Mungu na omba Roho Mtakatifu akusaidie kuombea kama ipasavyo.
Kabidhi kwa biashara/kazi yako kwa Mungu
Tuombee soko sawa sawa Ufunuo 5:9-10
Kazi za kufanya. Mungu akupe mawazo ya kitu cha kufanya ili kukuongezea kipato.
Ombea akina Zakayo ili wasije wakatoza zaidi. Maana kama wako akina Zakayo katika mfumo wa kodi na wanatoza zaidi ili Mungu atusaidie wafanye kazi vizuri bila kutoza zaidi na kuomba rushwa.
Chukua agenda hizi nenda nazo kwa Mungu na omba Roho Mtakatifu akusaidie kuombea kama ipasavyo.
Maoni
Chapisha Maoni