Somo: Yesu akikutuma anakupa na nyenzo za kazi

 Bwana Yesu asifiwe mtu wa Mungu leo tutafakari juu ya namna ambavyo Yesu hutuma watumishi wake.



Msingi wa Somo letu utajengwa kutokra kitabu Cha Luka 9:1-2

Katika kitabu hichi tuna elezwa ya kwamba Yesu alikuwa na wanafunzi wake. Naalisukumwa ndani yake kuwatuna wanafunzi wake ndani ya ulemji ambao walikuwepo.na alipo watuma Kuna vitu aliwapa vya kuwasaidia katika Huo utumishi ambao alitaka wakaufanye biblia inasema.

Luka 9:1-2

[1]Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi.

[2]Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, na kupoza wagonjwa.

Ukiangalia hapa majukumu yalio kuwa mbele yao ni mawili 

  1. Kutangaza ufalme wa Mungu (kueneza)
  2. Kuponya wagonjwa.
Kutokana na Mambo hayo mawili waliyotakiwa kuyakamilisha na ili wayakamilishe vizuri  kwa mafanikio walipaswa  wapewe vitu viwili

  1. Uweza wa Mungu
  2. Na mamlaka
  •  juu ya mapepo na
  •  Magonjwa.

Tuanze kwa kutafakari juu ya mamlaka.

Neno mamlaka (authority) maana yake kutawala, kuongoza , kuendesha (controller) ,Unaposikia mamlaka ya Hali ya hewa maana nichombo ama taasisi Ina toa muongozo ama kusimamia na kufuatilia maswala ya Hali ya hewa , Unaposikia mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) inamanisha nitaasisi halali unayohusika na ukusanyaji wa mapato, kutoa muongozo walipaji wa mapato na kuendesha  shughuli za  ukusanyaji wa mapato.

Hizo ni mfano tu wa baadhi ya mamlaka zilizopo hapa nchi Tanzania.

Nini nataka tujifunze nataka ufahamu sio mamlaka zote zenye uwezo wakuku chukulia hatua endapo  utakaidi muongozo yao ama maelekeze.

Mfano.

Mamlaka ya Hali ya hewa haiwezi kukukamata Kama utahatarisha Hali ya hewa ya inchi kwa hivyo Basi katika vile vitu viwili uweza  na mamlaka hii taasisi Ina mamlaka haiana uweza na kwamaana hiyo haiwezi kusimamia indapo hakuta kuwana utii wa maelekezo yake.

Maoni