Leo tujifunze jinsi ambavyo nguvu za Roho wa Mungu, Roho Mtakatifu ambavyo nguvu zake Zina fanya kazi ndani yetu.
Tukisoma katika kitabu cha
1 Mambo ya Nyakati 16:11
[11]Mtakeni BWANA na nguvu zake;
Utafuteni uso wake siku zote.
Biblia inaweka msisitizo juu ya kumuhitaji Mungu na nguvu zake, na sisi tuna jua kuwa unapo okoka kwa mara ya kwanza amakwamara nyingine, Roho Mtakatifu anaingia ndani yako,lakini swala la kupokea nguvu nihatua nyingine ambayo tuna pewa Kama tunahitaji kwamaana nyingi Kama huoni umuhimu wakua na nguvu za Roho Mtakatifu haulazimishwi japoa uana shauri wa uwenazo kwa maana Zina faida zake.
Biblia inatuambia wanafunzi wa Yesu walijazwa nguvu za Roho Mtakatifu Siku ya Pentekoste , lakini tuna fahamu walikuwa wanatembea na yesu kwa kipindi Cha miaka mitatu, kwa hiyo Yesu walikuwa naye Ila nguvu za Roho wake hazi kuwepo ndani yao
Faida za Roho Matakatifu na nguvu zake
Zinakusaidia kushinda hila za adui
Matendo ya Mitume 13:7-12
[7]mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu.
[8]Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani.
[9]Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho,
[10]akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?
[11]Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza.
[12]Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.
Hili Jambo tuna liona hapokwa kwenye msisitizo mastari wa 9 kwamba Paulo akijaa Roho Matakatifu maana kulikuwa na nguvu za Roho Matakatifu lasivyo biblia isinge sema Mana tujua wazi kwamba Paulo alikuwa amaokoka na ni mtumishi wa Mungu aliepakwa mafuta kutokana na maandiko yanavyo tueleza habari za kukoka kwa Paulo kwa hiyo ilikuwazi kwamba Paulo alikuwa na Roho Matakatifu , lakini bado biblia ilitaka tujue kwamba saa hile kilichokuwa kinamsukuma ndani ni nguvu za Roho matakatifu. Mana biblia ingeweza kunyamaza nabado tunge amini alikuwa ni Roho Matakatifu Ila wameandika hiyo ilitupate kujua kwamba hakuwa Paulo Bali alikuwa ni Roho wa Mungu aliye kuwa akipambana akitikea ndani ya Paulo .
2.Nguvu za Roho Mtakatifu zinakupa ujasiri ndani yako.
Matendo ya Mitume 4:8-13
[8]Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli,
[9]kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu, jinsi alivyoponywa,
[10]jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu.
[11]Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni.
[12]Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
[13]Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.
Hapo tuna muona Petro akiwa katika malumbano na na makuhani walicho kuwa wanakitaka nikumnyamazisha Petro , lakini biblia ina sema akijaa Roho Matakatifu aliweza kuwa na hekima yamna ya kuwajibu bila ya kuogopa amakuvunja Sheria kitu ambacho kilifanya wakose sababu ya kumkamata lakini kilicho wastajabisha zaidi niule ujasiri aliokuwa nao ndani yake.

Maoni
Chapisha Maoni